Mliberia Yanga anatafutwa Ulaya HABARI KAMILI IPO HAPA

Mshambuliaji hatari wa Simba, Kpah Sherman.
Na Saleh Ally
WAKATI Yanga ikiwa katika maandalizi ya mwisho kuwavaa Azam FC katika mechi ya Ligi Kuu Bara, jambo jipya limeibuka kuwa yule mshambuliaji wake hatari, Kpah Sherman raia wa Liberia, anatuhumiwa kutoroka kazini nchini Cyprus.

Taarifa kutoka Cyprus barani Ulaya kwa mmoja wa Watanzania wanaoishi nchini humo zimeeleza vyombo vya habari nchini humo, vimeripoti kuwa Mliberia huyo atafunguliwa mashitaka baada ya kutorokea Tanzania.“Nimesikia huyo mchezaji yuko huko nyumbani, ila huku vyombo vya habari vya hapa vimeripoti timu yake ina mpango wa kufungua kesi Fifa kuelezea kuhusiana na kutoroka kwake,” alisema Mtanzania huyo anayeishi nchini humo.
Juhudi za kuwapata viongozi wa Yanga ilikuwa ni ‘sheedaa’, imeelezwa Mwenyekiti Yusuf Manji yuko nje ya nchi na katibu mkuu mpya, hajaingia ofisini rasmi.Uongozi wa Klabu ya Centikaya TSK ya Cyprus, umethibitisha kushitushwa na taarifa za Sherman kuondoka nchini humo akidai ana matatizo ya kifamilia.
Lakini baadaye ukapata taarifa kuwa amejiunga na klabu kongwe ya Tanzania iitwayo Yanga nao wakaanza mipango ya kufungua mashitaka kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
Akizungumza na Championi Jumatano kutoka Cyprus, Rais wa Centikaya TSK, Meric Erulku amesema ni kweli kumekuwa na hali kutoelewana.“Kweli hali hiyo imetokea, hatukuambiwa kama anakwenda kwenye majaribio na ruhusa aliyopewa haikuwa ya kwenda kufanya majaribio.
“Kweli tuna mkataba naye, haujaisha na haujavunjwa. Pia hatujalipwa na kulikuwa na mpango wa kwenda Fifa, lakini meneja wake amezungumza nasi.“Hivyo tunaendelea na hayo mazungumzo ili kujua tutafikia wapi. Kwa kuwa hapa katikati kuna sikukuu, naomba unitafute Jumanne ijayo nitakupa jibu sahihi kama tunakwenda Fifa au tumemalizana nao,” alisema Erulku maarufu kama Buzlat.
Sherman amejiunga na Yanga kwa mkataba wa miaka miwili akichukua nafasi ya Mganda Hamis Kiiza.
Tayari Sherman ameichezea Yanga mechi moja ya kirafiki dhidi ya Simba ambayo Yanga ililala kwa mabao 2-0.Hata hivyo, Mliberia huyo ameonekana kukonga nyoyo za mashabiki kiuwezo baada ya mechi hiyo moja.

0 comments: