TIBAIJUKA ASEMA BAADA YA RAIS KIKWETE KUNIFUKUZA KAZI SASA NIPO JIMBONI KWANGU KUTATUA KERO ZA WANANCHI WANGU SOMA HAPA


Baadhi ya wananchi mkoani Kagera wamepinga  uamuzi   wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk Jakaya Mrisho Kikwete  kwa kumuondoa madarakani waziri wa ardhi nyumba na makazi   na kuwaweka kiporo viongozi wengine walioshiri kuhujumu pesa za akaunti ya Tegeta Escrow.

 
Wakiongea  na mwandishi mwetu, wananchi wa mkoa huo wamesema hawajajua  nini hatima ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. kikwete kwa kuwaweka Kiporo mawaziri wengine  waliohusika katika sakata hilo   na kumuuondoa waziri  Tibaijuka   na pia wamebaki na sintofahamu  ambapo wamemtaka  Rais  kutoa ufafanuzi kuwa licha ya kumng’oa madarakani kiongozi huyo  Je, Pesa  hizo zitarudishwa kwenye akaunti hiyo  ya Tegeta Escrow au la.
 
Nao baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa vya mkoa huo akiwemo katibu  wa siasa na uenezi wa Chama cha Mapinduzi  mkoa wa Kagera Hamimu Mahamudu amepongeza uamuzi wa Rais alioutoa   wakati  akiongea na wazee wa jijini Dar es salaam  kwa kumuondoa kiongozi huyo.
 
Kwa upande wake, katibu wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema  katika manispaa ya Bukoba Victor Sherejei akisema kuwa Rais hajatoa uamuzi sahii ambapo amemtaka  Rais kuwafahamisha watanzinia kuwa Pesa za Escrow zitarudishwa  lini katika akaunti hiyo au kuwaondoa viongozi hao madarakani ndio suluhisho  na kwamba pesa hizo hazirudishi?.
 
Kwa upande wake  aliyekuwa Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Profesa Anna Tibaijuka amesema  licha  ya Rais kumuondoa katika nafasi yake aliyokuwa nayo sasa amerudi jimboni kwake kwaajili ya  kutatua kero na changamoto mbalimbali za wananchi wake kwani nafasi aliyokuwanayo ilikuwa haimpi nafisi  ya  kuwasimamia wananchi katika jimbo lake na kwamba Pesa hizo alizopewa na Rugemalila zilikuwa za kusaidia shule na alipewa kama zawadi bila kujua kama  pesa hizo zilitoka katika akaunti ya Tegeta Escrow ndo maana hakutaka kujiuzulu.


0 comments: