Safari ya vijana wa 3 kutoka nzega waliotembea siku 37 kufikisha ujumbe kwa Rais Kikwete wakamatwa na polisi

 Vijana watatu kutoka  nzega wametembea kwa miguu kwa siku 37  hadi jijini dar es saalam kwa lengo la kutaka kwenda kumuona Rais Jakaya Kikwete kufikisha malamiko yao ikiwenmo kukithiri kwa vitendo vya rushwa na ubadilifu wa rasilimali za umma lakini safari ya vijana hao ikaishia mikononi mwa polisi baada ya kukadi agizo halali la  mkuu wa wilaya ya kinondoni Mh. Jordan Rugimbana la kuwataka wafuate taratibu za kumuona kiongozi huyo wa nchi.
Vijana hao ambao  walivamia magunia na kusema kuwa wamevaa hivyo ikiwa ni ishara ya kuonyesha uchungu wa namna ambavyo rasilimali za taifa zisivyowanufaisha wazawa.
 
Baadhi ya wananchi walioshuhudia  matembezi hayo  wamewataja vijana hao kama ni wazalendo ambao ujumbe wao unawagusa mamilioni ya watanzania ambo hawana ujasiri na uwezo wa kufanya kitendo cha  kijasiri kama hicho.
 
Baada ya vijana hao kufika kwa mkuu wa wilaya walifanya mazungumzo naye ambapo mkuu huyo aliwtaka wafuate taratibu za kumuona  rais na kusisitiza kuwa matembezi hayo yalipaswa kuishia hapo.
 
Kufuatia maagizo hayo vijana hao hawakukubaliana na agizo  hilo na kusema wao bado ni yao ya kwenda ikulu Ipo pale pale na ndipo walipioanza safari nyingine kuelekea huko na kabla ya hapo walitoa matamko yao mbele ya ofisi ya mkuu wa wilaya kablya ya kukamtwa na kupelekwa kituo cha polisi magomeni.
 

0 comments: