Kama Seif hataki Serikali mbili Ajiuzulu - Nape SOMA HAPA
Katibu wa NEC itikadi na uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM,Ndugu Nape Nnauye.
Watanzania
wametahadharishwa kutowasikiliza wanasiasa wenye nia ya kuvunja
muungano wa Tanganyika na Zanzibar, kwani katika kipindi cha miaka 51 ya
Muungano huo, kumekuwa na mafanikio kwa pande zote mbili
kauli
hiyo imetolewa na mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM mkoa wa
Magharibi Unguja, bwana Yusufu Mohamedi Yusufu, wakati akiwakaribisha
kuhutubia mkutano wa hadhara, viongozi wa juu wa chama hicho,
wanaoendelea na ziara katika visiwa vya unguja na pemba, ambapo
amewatahadharisha watanzania kutokubali hadaa za wanasiasa wenye nia ya
kuvunja muungano kwa maslahi yao binafsi,.
Akizungumza
katika mkutano huo Katibu wa CCM itikadi na uenezi wa CCM Nape Nnauye
amemtaka Makamu wa kwanza wa Rais ambaye pia ni katibu Mkuu wa CUF taifa
Maalim Seif Sharif Hamad ajiuzulu nafasi hiyo kama hataki Muungano wa
Serikali mbili.
Nape
amepinga kauli ya katibu mkuu wa chama cha wananchi CUF aliyodai haina
mashiko kufuatia chama cha CUF kudai kuchukua majimbo 18 ya uwakilishi
na ubunge katika uchaguzi ujao na kudai kuwa wamejipanga kushinda kwa
kishindo katika uchaguzi huo, kauli inayoungwa mkono na katibu mkuu wa
chama hicho komredi Abdulrahman Kinana.
Wakihutubia
wananchi waliofurika katika uwanja wa Tomondo baadhi ya viongozi wa
chama hicho walioambatana na katibu mkuu upande wa Zanzibar wakiwemo
wabunge wa bunge la jamuhuri ya mungano wa Tanzania na wawakilishi wa
baraza la wawakilishi la serikali ya mapinduzi Zanzibar wamesihi
wazanzibar kuipigia kura ya ndiyo katiba iliyopendekezwa muda utakapo
wadia.
0 comments: