Mh. John Mnyika awasilisha udhaifu wa mchakato wa mabadiliko ya katiba kwa katibu wa bunge
Mbunge
wa jimbo la Ubungo Mh John Mnyika amewasilisha kwa katibu wa bunge
taarifa ya hoja binafsi kuhusu kile alichodai kuwa ni udhaifu wa
mchakato wa mabadiliko ya katiba ili bunge lijadili udhaifu wa ukiukwaji
wa sheria katika mchakato huo ili lipitishe azimio la kuahirisha
mchakato huo mpaka madhaifu ya msingi yatakaposhughulikiwa.
Akizungumzana
na mtandao huu katika ofisi za bunge Mh Mnyika pia amemtaka rais wa
jamhuri ya muungano wa Tanzania kuheshimu makubaliano ya viongozi wa
vyama vya siasa kwa kuwa kuendelea na mchakato huo si tu kukiuka
makubaliano ya TCD bali pia ni kukiuka sheria zilizouanzisha mchakato
huo.
0 comments: