ZARI HAWEZI KUZAA NA DIAMOND, MUME AANIKA SIRI NZITO!
Oohoo! Wakati
staa mkubwa wa muziki wa Afro-Pop, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’
akichekelea kitendo cha mpenzi wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’ au
‘The Boss Lady’ kunasa mimba yake, habari ya mjini huko Kampala, Uganda
ni juu ya aliyekuwa mume wa mwanamama huyo,
Ivan Ssemwanga kufunguka na kusema: “Naapa Zari hawezi kuzaa na Diamond.”HABARI YA MJINI
Wikiendi
iliyopita, vyombo vya habari na mitandao nchini Uganda ambako kuna
makazi mengine ya Zari mbali na Afrika Kusini, kulipambwa na habari hizo
baada ya mwanaume huyo aliyezaa na mwanamama huyo watoto watatu kuanika
siri nzito juu ya ishu hiyo.
‘Ubuyu’
huo ulidadavua kwamba, kwanza jamaa huyo mwenye utajiri wa kutupwa
alianza kwa kuelezea namna alivyoshtuka aliposikia Zari ni mjamzito.
Alisema
kwamba alishangaa kusikia Zari ni mjamzito wakati ana umri wa karibia
miaka 40 na watoto watatu ambao amekuwa akiwapuuza na kuendelea kuzurura
na mpenzi wake mpya, Diamond sehemu mbalimbali ndani na nje ya Bara la
Afrika.
0 comments: