MAITI YASAFIRISHWA JUU YA KERIA INGIA HAPA

0 comments
Jeneza lenye mwili wa marehemu likiwekwa vizuri kwenye keria ya gari tayari kwa safari.

DUNIANI kuna matukio! Tofauti na utaratibu uliozoeleka, katika hali ya kushangaza, wanandugu wamelazimika kusafirisha maiti juu ya keria ya basi kutoka Arusha hadi Lushoto, Tanga kutokana na ukata.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni ambapo chanzo kilieleza kuwa, wanandugu hao ambao hawakuwa tayari kuanika majina yao, walifikia hatua hiyo ili waweze kuenea kwenye basi moja aina ya Toyota-Coaster kwenda Lushoto, mkoani Tanga.
Waombolezaji wakiupandisha mwili wa marehemu (ndani ya jeneza) juu ya gari.

“Waliona kama wangeweka maiti ndani ya gari, wangelazimika kutoa siti mbili hivyo wasingetosha, baadhi ya ndugu walishauri kwamba mwili wa marehemu uwekwe juu ya keria ili waombolezaji waweze kuenea,” kilisema chanzo.
Chanzo hicho kilizidi kushusha data kuwa, kabla ya wanandugu kukubaliana kusafirisha juu ya keria mwili huo, uliibuka ubishani mkubwa kwani kuna baadhi waliafiki kitendo hicho lakini wengine hawakuafiki.“Kuna ambao walikataa na kusema si jambo la busara kuiweka maiti juu ya keria lakini mwisho wa siku walizidiwa kwa hoja na wale walioshauri iwekwe juu kwani tatizo lilikuwa kwenye fedha za kukodi gari jingine.

“Walishajikusanya kusanya hadi dakika za mwisho, fedha walizopata zilitosha kukodi gari moja hivyo hawakuwa na jinsi japo ambao hawakuafiki, walihofia kuwa huenda wasifike salama huku wengine wakichungulia pembeni kila wakati wakihofu huenda jeneza linaweza kuanguka,” kilisema chanzo hicho.
Hata hivyo pamoja na kutofautiana huko kwa wanandugu, walifanikiwa kusafiri salama hadi Lushoto na kufanikiwa kumpumzisha mpendwa wao.

Read More »

Dk Slaa kupanda ‘kizimbani’ leo SOMA HAPA

0 comments


Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibroad Slaa, leo anatarajiwa kupanda kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Hai kutoa ushahidi katika kesi ya jinai inayomkabili kijana aliyejifanya Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Wilaya ya Hai, Dennis Mpelembwa alisema jana kuwa Dk Slaa amethibitisha kuitikia wito huo wa Mahakama.
Katika ushahidi uliotolewa mahakamani, Dk Slaa akiwa Mtendaji Mkuu wa Chadema, ndiye anayedaiwa kushughulikia suala la mshtakiwa kutaka kuwatapeli viongozi wa Chadema.
Tayari Jaji Samatta na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema wamekwishatoa ushahidi wao katika kesi hiyo inayoendeshwa na mawakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).
Katika ushahidi wake, Jaji Samatta alikana kumfahamu mshtakiwa Abeid Adam Abeid (22) na kwamba namba ya simu iliyotumiwa kujitambulisha kwa Dk Slaa na Lema kuwa ni Jaji Samatta siyo yake.
Kwa upande wake, Lema alidai mshtakiwa huyo alimtumia meseji mbalimbali akijitambulisha kwake kuwa ni Jaji Samatta na kwamba angemsaidia katika rufaa yake ya kuvuliwa ubunge ya mwaka 2012.
Upande wa mashtaka, ukiongozwa na Wakili wa Takukuru, Susan Kimaro ulidai mshtakiwa alitenda kosa hilo kati ya Aprili na Mei 2012. Mtuhumiwa alikana mashtaka hayo na leo upande wa mashtaka unatarajiwa kufunga ushahidi wao baada ya Dk Slaa na shahidi mwingine ambaye hajatajwa, kutoa ushahidi wao.

Read More »

Baada ya anna tibaijuka kuchafuka kisiasa ona halima mdee alivyomponda

0 comments



























Read More »

Kingunge: Waliojitokeza kuwania urais CCM hawana sifa

0 comments


Mwanasiasa mkongwe nchini Mzee Kingunge Ngombare Mwiru akizungumza na wanahabari

Harakati za kuwania urais ndani ya CCM zimeingia katika hatua mpya baada ya mwanasiasa mkongwe, Kingunge Ngombale - Mwiru kuibuka na kudai kuwa wote waliojitokeza kuwania nafasi hiyo hawana sifa kwa kuwa wanatumia fedha kutaka kuingia Ikulu.
Kauli ya mwanasiasa huyo ambayo imekuja siku moja kabla ya Kamati Kuu ya CCM kukutana leo mjini Unguja na moja ya ajenda ikitajwa kuwa suala la maadili, inaweza kuwa mwiba mchungu kwa wanasiasa hao ambao wanaongezeka kila kukicha.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Kingunge alisema: “Kuna suala la kukosa uadilifu, kuna suala la matumizi ya pesa na nikwambie ukweli, hao wanaotangaza urais wote wanatumia pesa, wanatumia faulo mbalimbali na wananchi wanajua.”
Kwa miezi kadhaa sasa, baadhi ya makada wa CCM wamekuwa wakitajwa kufanya harakati kichinichini na wengine kushiriki shughuli za wazi zinazoashiria kuwa wanataka kuwania nafasi hiyo ya juu. Hadi sasa makada wanne tayari wameweka wazi nia yao hiyo.
Hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, January Makamba kwa nyakati tofauti walitoa kauli zinazowashutumu makada wengine wa chama hicho kwa matumizi makubwa ya fedha katika kushawishi uungwaji mkono.
Hata hivyo, kauli za wanasiasa hao zimedaiwa kuwa ni fitina za kisiasa kwa kuwa wagombea wote wanatoa fedha, bali wanazidiana viwango tu.
Mbali na Makamba na Membe, wanaCCM wengine waliotangaza au kutajwa kuwania urais ni Mbunge wa Nzega, Dk Khamis Kigwangalla, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.
Wengine ni mawaziri wakuu wa zamani, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wasira na aliyewahi kuwa Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.
Kauli ya Kingunge aliyoitoa kupitia Televisheni ya ITV, imekuja wakati wanasiasa sita miongoni mwa hao wanaotajwa wakikaribia kumaliza miezi 12 ya uangalizi kutokana na onyo kali dhidi yao lililotolewa na Kamati Kuu ya CCM Februari 18, mwaka jana baada ya kuwatia hatiani kwa makosa ya “kuanza kampeni mapema na kufanya mambo ambayo ni kinyume na maadili ya chama na ya jamii.”
Wanaotumikia adhabu hiyo ni Lowassa, Sumaye, Njeleja, Makamba, Wasira na Membe.
Akisisitiza hoja yake hiyo bila kutaja majina, Kingunge alisema makada hao wamekuwa wakitumia fedha nyingi kujitangaza na kutengeneza ushawishi wa kukubalika kwa wananchi jambo ambalo ni kinyume na maadili ya uongozi.
Kingunge alisema mwanasiasa yeyote anayehitaji uongozi hapaswi kutumia fedha kushawishi wananchi wamchague.

Read More »

VIGOGO WIZARA YA UJENZI WAMKIMBIA MAGUFULI!

0 comments


 Waziri ya Ujenzi Dk. John Pombe Magufuli.
Baadhi ya vigogo katika Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Dk. John Pombe Magufuli (pichani), wameikimbia wizara hiyo na kwenda sehemu nyingine kwa kile walichodai ni uongozi wa kibabe na unyanyasaji katika idara ya usalama barabarani na mazingira.
Uchunguzi uliofanywa na paparazi wizarani hapo umebaini kuwa katika idara hiyo inayoongozwa na Julius Chambo kama Kaimu Mkurugenzi imekimbiwa na vigogo watatu, Juma Kijavara, Omari Kinyange na Samson Nkundineza ambao wameondoka wizarani hapo ndani ya mwezi mmoja, Desemba mwaka jana.
Vyanzo vyetu vya habari ndani ya wizara hiyo vinadai kwamba tangu Chambo ahamishiwe katika idara hiyo akitokea kituo cha mizani Himo mkoani Kilimanjaro, utendaji wa kazi umekuwa ukisuasua kwa kile kinachodaiwa kuwa ni uongozi wa kidikteta pia wameona kama amewekwa hapo kiupendeleo kwa vile mambo ya utawala hajui.
Katika idara hiyo inayoongozwa na Chambo ilikuwa na wahandisi wanne lakini baada ya kuondoka kwa hao watatu alibakia mmoja na inasemekana wameletwa wengine kufidia walioondoka.
Kuhama kwa vigogo hao kumewatia hofu wafanyakazi waliobaki na inasemekana kuwa baadhi yao wanataka kuondoka.
Aidha baadhi ya wafanyakazi wamelalamikia kipindi kirefu alichopewa kukaimu nafasi hiyo.
“Huwezi kukaimu ofisi kwa muda mrefu namna hiyo  hapa kuna tatizo,” alisema mhandisi mmoja kwa sharti la kutoandikwa jina lake mtandaoni.
Aliongeza kuwa kama wizara haitafanya mabadiliko stahiki kuna wahandisi watatu wataondoka hivyo wizara kupoteza wataalamu wazoefu kitu ambacho kitaleta shida kubwa wizarani hapo.
paparazi alipomtafuta Chambo ofisini kwake alikiri kuondoka kwa vigogo hao na akadai kuwa ni mmoja tu ndiye aliyemuaga lakini wengine hawakufanya hivyo.
“Mimi naamini wameondoka kwenda kutafuta maslahi zaidi, kuhusu madai mengine mimi siwezi kuzungumzia masuala ya wizara, nendeni kwa katibu mkuu,” alisema Chambo. Naye katibu mkuu wa wizara hiyo, Musa Lyombe alipohojiwa alisema wafanyakazi hao wameondoka Desemba mwaka jana lakini hata yeye ameshangazwa na kuondoka kwao.
“Nafikiri kuna jambo na kuna umuhimu wa kulichunguza suala hili kwa karibu, wao walikuja kwangu nikijua wanafuata maslahi, kwa nini itokee katika idara hiyo moja?” alihoji.

Read More »

SHAMSA: NALALA NA MUME WANGU LOKESHENI

0 comments


Staa wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford.
STAA wa filamu za Kibongo, Shamsa Ford amesema kuwa mara kadhaa anapokuwa lokesheni akishuti filamu mume wake, Dickson Matoke huwa anamfuata na kulala naye hadi asubuhi huku akiamini kufanya hivyo kunachangia kutochepuka.
Akizungumza na paparazi, Shamsa alisema kuwa kitendo cha mumewe kumfuata haina maana kwamba wanavunja sheria zao bali hilo analifanya kwa kuwa yeye ni mke wa mtu na huwa anapewa chumba chake maalum.
“Mara nyingi ninapokuwa lokesheni kama si mbali na nyumbani basi naenda kumuona mume wangu na mtoto lakini kama ni mbali kidogo mume wangu huwa anakuja na kulala na mimi chumbani kwangu, asubuhi anaondoka naendelea na kazi yangu,” alisema Shamsa.

Read More »

AJALI YA GARI YAUA WATATU KOROGWE

0 comments
 



AJALI hii mbaya ilitokea juzi (Jumapili) katika Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga ambapo watu watatu wanadaiwa kupoteza maisha.
Dereva wa gari hili lililopata ajali amelazwa katika Hospitali ya KCMC, Moshi akiendelea na matibabu.

Read More »

Picha na Orodha ya washindi wa tuzo za FIFA Ballon d’Or 2014.

0 comments


cr 2

Tuzo za Ballon d’Or zimefanyika 12 Jan 2014 ambapo wachezaji bora wa mwaka wamepokea tuzo kutoka shirikisho la soka ulimwenguni FIFA Kupitia Fifa Ballon d’Or.
Tuzo ya mchezaji bora duniani imeshindwa na Cristiano Ronaldo, alikuwa akiwani na Lionel Messi na mlinda mlango Manuel Neur.
Cristiano Ronaldo ameshinda kwa asilimia 37.66 ya kura zote akimshinda Lionel Messi  mwenye asilimia 15.76% na Manuel Neuer mwenye asilimia 15.72%.
Tuzo ya goli bora ameshinda James Rodriguez .

Tuzo ya mwanasoka wa kike ameshinda Nedine Kassler.
Tuzo ya mlinda mlango bora ameshinda Manuel Neur .
Tuzo ya kocha bora ameshinda mjerumani Joachim Law  .
Kikosi bora cha FIFA kimetajwa kuwa na hawa wachezaji . Neuer; Lahm, Ramos, David Luiz, Thiago Silva; Di Maria, Iniesta, Kroos; Messi, Ronaldo, Roben
cr 1
ronald

Read More »

Watatu wafukiwa na kifusi wakichimba madini wilayani Kahama mkoani Shinyanga

0 comments




Wachimbaji watatu wa madini ya dhahabu ya Kalole kata ya Lunguya wilayani Kahama mkoani Shinyanga  wamefariki dunia baada ya kufukiwa na udongo wakiwa kwenye shimo la dhahabu wakitafuta dhahabu.

Kwa mujibu wa taarifa ya kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Januari 7,2015 saa 12 asubuhi katika machimbo madogo ya dhahabu ya Kalole kata ya Lunguya,tarafa ya Msalala wilayani Kahama.

Aliwataja waliofariki kwa kufukiwa kwenye shimo  hilo la dhahabu kuwa ni  Kulwa Magele(20) mkazi wa Shishani wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, Ihalu Maheme(23) mkazi wa Idisa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu na Lameck Frank(22) mkazi wa Nzega mkoani Tabora.

Kamanda Kamugisha alisema vijana hao ambao ni wachimbaji wadogo wa madini waligundulika wakiwa wamekufa ndani ya shimo la kuchimbia dhahabu na inaelezwa kuwa waliingia kwenye shimo hilo ambalo halitumiki kwa nia ya kuchimba dhahabu ndpo likabomoka na kuwafukia na kusababisha  vifo vyao papo hapo.
Wakati huo huo mwanamke aitwaye Sayi Shitunguru(50) mkazi wa  kijiji cha Buruma kata ya Isaka wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kupigwa kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika akiwa nyumbani kwake.

Kamanda Kamugisha alisema tukio hilo limetokea Januari 7,2015 saa 1 asubuhi ambapo mwanamke huyo akiwa nyumbani kwake alivamiwa na mtu/watu wasiojulikana kasha kumpiga na kitu kizito kichwani na kusababisha kifo chake papo hapo.

Alisema chanzo cha tukio hilo bado hakijajulikana  na jeshi la polisi linaendelea kufanyan uchunguzi ili kubaini chanzo chake.

Hata hiyvyo alisema tayari wanamshikilia mtu mmoja aitwaye  John Jota(33) mkazi wa Kazungu wilayani Kahama kwa mahojiano zaidi huku akiwataka wananchi kushirikiana na polisi ili kusaidia kukamatwa kwa wahusika wa mauaji hayo.

Read More »

Kuhusu Ajali aliyopata Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.

0 comments
Leo January 10 kupitia mitandao na blogs tofauti zimeenea taarifa na picha za ajali ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi. Taarifa nilizopokea mpaka sasa kuhusu ajali hii ni kwamba mhe Mbilinyi amepata ajali akielekea Dar es salaam kwenye kona kali iliyopo eneo la Kitonga, Iringa akiwa na watu wanne kwenye gari moja.
vyombo vya habari vimesema hakuna mtu aliyepoteza maisha waka kupata majeraha yeyote makubwa. Kamanda wa Polisi wa Iringa, Ramadhani Mungi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo leo.
sugu 1 
 sugu 2 
 sugu 3 
 sugu 4 
 sugu 5 
 sugu 6


Read More »

Ifahamu klabu pekee inayoweza kumsajili Messi kwa sasa… INGIA HAPA

0 comments
lionel_messi_barcelona

Huku habari kuhusu uhusiano mbaya wa Lionel Messi na klabu yake ukiendelea kutengeneza headlines kwenye vyombo vya habari barani Ulaya tetesi za kuondoka kwake zimezidi kushika kasi huku kila siku ikiibuka story mpya.
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na mtaalamu wa biashara kwenye mchezo wa soka ni klabu mbili pekee ambazo kwa sasa zina uwezo wa kumsajili nyota huyu raia wa Argentina kinyume na ilivyoripotiwa kuwa klabu kadhaa ziko kwenye harakati za kumsajili.
Klabu hizi zimetajwa kuwa Manchester United na Real Madrid kutokana na kuwa na msuli wa kifedha pamoja na sababu nyingine ambazo zinaleta ugumu kwa zile klabu ambazo zinaweza kuwa na fedha lakini zikashindwa kufanya usajili kutokana na kubanwa kwenye sehemu tofauti.
Katika hali ya kawaida klabu kama Manchester City, PSG , Chelsea na Bayern Munich zinaweza kumsajili mchezaji yoyote kwa bei yoyote, lakini hali kwa sasa ni tofauti kwani kanuni za kusimamia matumizi ya fedha kwa vilabu ‘Financial Fair Play’ zinafanya matumizi kwa vilabu yafanywe kwa kuzingatia vitu vingi.
Hapa ndio mahali ambako United na Real zinapata faida endapo zitakuwa na dhamira ya kumsajili Messi.
Ili kumnunua Messi klabu inayomtaka itapaswa kulipa ada ya uhamisho ambayo ni paundi milioni 196 na mshahara wake utalazimika kuwa mkubwa kutokana na hadhi ya mchezaji mwenyewe na kwa mantiki hiyo ni United na Madrid pekee ambazo zinatengeneza aina ya fedha ambayo inaweza kutosha kumnunua Messi pasipo kukiuka sheria za Financial Fair Play.
Klabu ambazo zinatangaza hasara ya zaidi ya paundi milioni 23.5 kwa muda wa miaka mitatu zinaadhibiwa na sheria za FFP na tayari Man City na PSG zimekumbana na rungu hilo jambo ambalo linawaondoa kwenye mbio za kumsajili Messi endapo nyota huyo atawekwa sokoni.
Pamoja na ukweli huu bado haitakuwa rahisi kwa Barcelona kukubali kumuona Messi akiondoka hasa ukizingatia kuwa klabu hiyo ina adhabu ya kutofanya usajili kwa muda wa mwaka mzima hali inayowafanya wasiwe kwenye nafasi ya kumuuza mchezaji yoyote muhimu kwani kufanya hivyo itakuwa sawa na kujidhoofisha huku wakiwa hawana nafasi ya kujiimarisha.

Read More »

TAZAMA PICHA ALIZOPOSTI MCHUMBA WA NAY MTANDAONI INGIA HAPA

0 comments




Mchumba wa staa wa Bongo Fleva, Emanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' , Siwema Edson 'Mama Curtis' amepost leo picha za mahaba akiwa kitandani na mzazi mwenzie huyo kupitia Account yake ya Instagram.

Read More »

Man U yamsajili kipa wa Barcelona

0 comments

Victor Valdes akisaini kuichezea Man U.

MANCHESTER, England  
KLABU ya Manchester United imethibitisha kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona, Victor Valdes kwa mkataba wa mwaka mmoja na nusu.
Valdes mwenye umri wa miaka 32, alikuwa akifanya mazoezi na klabu hiyo tangu Oktoba, mwaka jana baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akisumbuliwa na maumivu ya goti.
Valdes ameeleza kuwa amefurahishwa na usajili huo na yupo tayari kufanya kazi na kipa chaguo la kwanza la timu hiyo, David de Gea ambaye ni raia mwenzake wa Hispania.

Read More »

Yanga yamtema Kaseja rasmi, yamdai 400m

0 comments


Kipa wa Yanga Juma Kaseja.

YANGA imetangaza rasmi kuachana na kipa Juma Kaseja lakini Championi Ijumaa linafahamu ukweli kuwa klabu hiyo imepanga kumfungulia mashitaka ya kumtaka alipe shilingi milioni 400, kutokana na kuvunja mkataba.
Akitangaza kwa waandishi wa habari jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa klabu hiyo Jerry Muro alisema kuwa Kaseja ndiye aliyevunja mkataba na klabu hiyo kutokana na kutoonekana mazoezini kwa zaidi ya saa 48, hivyo kuvunja kipengele katika mkataba wake.
“Yanga inatangaza rasmi kuwa haitakuwa na kipa Juma Kaseja kwa sababu amevunja mkataba na klabu yetu na tunamtakia kila la kheri katika maisha yake mapya  huko aendako,” alisema Muro
Kuhusu madai kuwa Kaseja anaidai Yanga, Muro alifafanua: “Kaseja alisaini mkataba na klabu Novemba 8, 2013, siku hiyohiyo akalipwa shilingi milioni 20, makubaliano ilikuwa alipwe shilingi milioni 40 ndani ya kipindi cha mkataba wake wa miaka miwili na hakukuwa na muda maalum uliopangwa.
“Januari 15, 2014 klabu ikamlipa fedha zake zilizosalia shilingi milioni 20, lakini Novemba 11, 2014, akaleta barua ya malalamiko kadhaa kwetu akidai hapati nafasi ya kucheza jambo ambalo siyo kweli na alilalamika kuhusu masuala ya bima.
“Desemba 15, 2014, Klabu ya Yanga ilimjibu barua hiyo na kumfafanulia kile alichohitaji, lakini yote kwa yote hakuna ambacho anatudai wala tunachomdai.”Baada ya hapo gazeti hili lilipata taarifa za ndani juu ya mpango huo wa Yanga kumshitaki Kaseja kwa kukiuka masharti ya mkataba, lakini alipoulizwa Muro alisema hajui chochote kuhusua suala hilo.

Read More »

DAH INASIKITISHA SANA : MWANAFUNZI WA DARASA LA TATU ABAKWA NA WATU MPAKA KUFARIKI DUNIA KISHA KUMUWEKA KWENYE SINKI LA KUOGEA-MBEYA

0 comments


MWANAFUNZI wa darasa la tatu katika Shule ya Msingi Rwanda Nzovwe jijini Mbeya , Elika Mkubwa (8), amefariki dunia baada ya kubakwa na watu wasiojulukana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi, alisema baada ya watu hao kufanya unyama huo, waliuweka mwili wa mtoto huyo katika sinki la kuogea kwenye nyumba moja ambayo haijakamilika ujenzi wake. Pamoja na hayo, alisema upelelezi bado unaendelea ili kuwabaini waliohusika na tukio hilo.
Akizungumza eneo la tukio, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.
Akizungumza eneo la tukio na paparazi huru, kiongozi wa Mtaa wa Ilomba, Ezekiel Mwakalandwa, alisema taarifa za mauaji hayo alizipata jana asubuhi kupitia kwa majirani zake.
"Nilipota taarifa hiyo, niliongozana na majirani tukiwa na ndugu wa marehemu na kushuhudia mwili wa mtoto huyo ukiwa umelazwa kwenye sinki la kuogea huku sehemu zake za siri zikiwa zimeharibiwa vibaya"
Mama mlezi wa mtoto huyo, Sala Mwandobo, alisema mtoto huyo alitoweka nyumbani kwake January 7 mwaka huu baada ya kuaga anakwenda kufua nguo za shule eneo la chemchem ya maji lililopo mbali kidogo na nyumbani kwake.

Read More »

Mume hanifikishi kisawasawa, Akimaliza yeye mimi nabaki bado na hamu INGIA HAPA KUSOMA HABARI KAMILI

0 comments


Mimi ni msichana wa miaka 27 nimeolewa miaka minne iliyopita na nina watoto wawili wote wa kike. Mwanzoni mwa mahusiano yetu na mume wangu (wakati tukiwa wachumba) na hata kama mwaka mmoja na nusu hivi kwenye ndoa yetu, baba watoto alikuwa ananiweza kweli....yaani nikikutana nae...aaah, allahmdullillah, nilikuwa naiona anga kwa uhalisia kabisa....na akiwa amechoka sana, basi hata mbili nitapata na kweli nilikuwa najisikia nime.....! Na kwa wiki nilikuwa napata kama siku nne hivi, yale mapigo ya sawa sawa.

Sasa kwa kipindi kama cha mwaka mmoja hivi...da, baba watoto kwa kweli ana underperform kabisa....wakati mwingine inapita wiki nzima, sionji na mimi mwanamke huwa nahitaji...nikimwambia anasema nimechoka sana kazini. Kwa heshima niliyo nayo kwa mume wangu, huwa namwambia sawa, lakini moyoni huwa nabaki na maswali mengi kuliko majibu. Huwa nahisi moja kati ya mambno haya:

1. Huenda mume wangu ameanza mambo ya nyumba ndogo, so akitoka kazini huenda anamalizia huko huko then akirudi nyumbani anakuwa hoi

2. Labda umbile langu limemchosha, coz kabla hatujaoana nilikuwa na bambataa ya wastani na kiuno chembamba, lakini now sio utani, nyonga imebaki vile vile lakini makalio yameongezeka mara-dufu, so huwa hafikii pale "Dar es Salaam" kisawasawa 

Haya yoye ni mawazo yangu ambayo ninayo moyoni. Sasa sijajua kama nimuulize au na mimi nianze kupiga show za nje kwani wanaonitongoza nikiwapanga kuanzia Dar, basi watafika hadi Morogoro......tatizo nampenda baba watoto na nimempa muda wa kama miezi 6 hivi, kama hatobadilika, basi nita-confirm namba moja ya hapo juu....So na mimi nitaanzia  kutafuta wa kurusha nae roho.

Read More »

Viongozi wa Siasa Wamcharukia Rais Kikwete…..Wamtaka Afanye Maamuzi juu ya Waziri wa Nishati na Madini.

0 comments

Viongozi wa vyama vya siasa nchini wamemtaka Rais Jakaya Kikwete kutekeleza ahadi yake aliyoahidi wakati wa mkutano na wazee wa Dar es Salaam ya kufanya maamuzi ya kumwajibisha waziri wa nishati na madini ambaye alimweka kiporo na kudai kuwa atatoa maamuzi ndani ya siku mbili lakini hadi leo amekaa kimya.
 
Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Prof Iibrahim Lipumba amesema suala la viongozi wakiwemo mawaziri kuwajibika halikuanza leo hasa anaposhindwa kutekeleza majukumu yake kikamilifu na kuisababishia serikali hasara au kushusha heshima ya taifa hivyo ni vyema uwajibikaji ukawa ni kwa kila mtumishi wa umma bila kubagua ili kuleta tija kwa taifa.
 
slaa
Dk. Slaa
Kwa upande wake mjumbe wa halmashauri kuu taifa ya chama cha mapinduzi CCM Bw Najim Msenga amesema niimani ya chama chake kuwa rais atafanya maamuzi sahihi kwa maslahi ya taifa kama alivyoahidi na kwamba suala hilo haliwezi kuathiri uhai wa CCM kwani bado iko imara baada ya baadhi ya watuhumiwa kuchukuliwa hatua.
 
Akizungumzia suala hilo katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Dk Willbroad Silaa amesema hata hao waliojiuzulu na kuenguliwa uteuzi wao maadam uchunguzi ulifanywa na vyombo sahihi hadi kufikia hatua ya kupelekwa bungeni na kujadiliwa na wao kutoa maazimio watuhumiwa wote hadi sasa walipaswa wawe wamefikishwa mahakamani.
 
Katika mkutano wake na wazee wa Dar es Salaam uliofanyika ukumbi wa Diamond Jublee desemba 22 mwaka jana Rais Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Mh Anna Tibaijuka na kutangaza kumweka kiporo waziri wa nishati na madini Prof Muhongo

Read More »

WANNE WAFA AJALINI IRINGA SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI

0 comments
Muonekano wa lori lenye namba za usajili T122 ALW baada ya kugongana na basi la Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD katika Kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
 
Basi la Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD baada ya ajali hiyo.
ZAIDI ya watu 4 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la abiria kutoka Mbeya kwenda Dodoma kugongana na lori katika Kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amesema kuwa ajali hiyo imetokea saa 4.45 asubuhi na kuhusisha basi mali ya Kampuni ya Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD kugongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T122 ALW mali ya Kampuni ya Transisco lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda nchi jirani.
Amesema watu wawili waliokuwa ndani ya basi wamefariki papo hapo na wote waliokuwa ndani ya lori wanahofiwa kufa, ambapo hadi kufikia  saa 7 mchana, watu wawili ndani ya lori walikuwa wamethibitika kufariki dunia na kufanya waliokufa kuwa wanne.

Zoezi la kuondoa miili iliyokuwa ndani ya lori linaendelea ambapo amesema kuwa huenda idadi hiyo ya waliokufa ikaongezeka.
Akielezea mazingira ya ajali hiyo, Kamanda Mungi amesema kuwa basi hilo lilikuwa likijaribu kulipita basi lililokuwa mbele yake katika eneo ambapo palikuwa na lori lingine lililoharibika, wakati huo huo lori lililohusika katika ajali hiyo lilikuwa likikwepa lori lililoharibika pamoja na basi hilo, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso katika jitihada za kukwepana.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mafinga, Iringa.

Read More »

Picha,Diamond Alivyokutana na Peter wa P Square na Fally Ipupa Nigeria. SOMA HAPA

0 comments
Unafuatilia habari za burudani Tanzania, basi utakumbuka swali waliloulizwa P Square walivyokuja Tanzania kuhusu kumfahamu Diamond. Jibu lao lilitengeneza drama kwa mashabiki wa Platnumz.
Diamond kwa sasa yupo Nigeria kwaajili ya tuzo za Glo-CAf. Amekutana na mastaa tofauti na miongoni mwao ni Peter wa P Square na Fally Ipupa.
diamond square
diamond pupa 2 diamond pupa 3 diamond pupa 4 diamond pupa 5 diamond pupa 6 diamond pupa

Read More »