CHADEMA YATOA TAMKO: Yaitaka Serikali kuwachukulia hatua waliohusika na wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
Chama
cha demokrasia na maendeleo-Chadema- kimeitaka serikali kuwachukulia
hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani viongozi waliohusika katika wizi wa
fedha katika akaunti ya Tegeta -Escrow- licha ya wengine kuandika barua
kujiuzulu wadhifa zao.
Akizungumza
na waandishi wa habari, naibu katibu mkuu wa Chadema, Mhe.John Mnyika
amemtaka rais Jakaya Kikwete kuyafanyia kazi maadhimio ya bunge ya
kuwaondoa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria viongozi hao, hata
kama watajiuzulu nyazifa zao.
Akielezea
uchaguzi wa serikali za mitaa, naibu katibu mkuu wa chama hicho
Zanzibar Bwana Salum Mwalimu amemtaka waziri wa tamisemi Mhe. Hawa
Ghasia kutangaza matokea chaguzi za serikali za mitaa kwa nchi nzima
badala ya kuwahachia viongozi wa vyama vya siasa kuendelea kuwadanganya
wananchi kuwa vyama vyao vimepata ushindi wa kishindo.
Kwa
upande wake baadhi ya wananchi wameitaka serikali kufuatilia ajira za
wageni katika baadhi ya benki nchni kutokana na ongezeko la wizi ambao
yanaambatana na baadhi ya watendaji kujiuzulu nyadhifa zao baada ya
muda.
0 comments: