VURUGU KUBWA YATOKEA MAKABURINI SHINYANGA, NDUGU WAPASUA MWILI WA MAREHEMU! SOMA HAPA


Habari tulizozipata hivi punde zinasema kuwa kumetokea vurugu za aina yake katika makaburi ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga wakati wa mazishi ya mwanamke mmoja aitwaye Benadetha Steven(35) aliyekuwa anaishi katika mtaa wa Mapinduzi maarufu mtaa wa Juma Matv katika kata ya Ndala aliyefariki dunia juzi wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Tukio hili limetokea mchana huu wakati wa mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kufariki dunia kutokana na uvimbe wa tumboni uliokuwa unamsumbua hivyo ndugu wa marehemu kuamua kumfanyia mambo ya kimila ili kuondoa mkosi katika ukoo wao.

Habari zinasema kuwa ndugu wa mwanamke huyo anayetokea Musoma (Mkurya) walikuwa wanataka ndugu yao apasuliwe tumbo wafanye mambo ya kimila makaburini lakini uongozi wa eneo husika wakasema utaratibu huo ungefanyika hospitalini badala ya hadharani watu wakishuhudia.

 Tunaambiwa kuwa mwanamke huyo alikuwa ameolewa Shinyanga na alipofariki mwili wake ulihifadhiwa katika hospitali ya mkoa wa Shinyanga.

Mgogoro huo ulianzia nyumbani kabla ya kwenda makaburini,ndugu walitulia na wakati mazishi yanaendelea ndipo ndugu wa marehemu wakaingia kaburini kuzuia wananzengo wasitupie udongo makaburini.

"Mchungaji alipomaliza ibada ya mazishi akaruhusu mwili uzikwe,wananzengo wakaanza kutupia udongo,ghafla ndugu wa marehemu wakaingia kaburini na kuzuia wananzengo,wakatoa mwili wakauchana kwa wembe,wakachinja kuku,wakamwagia damu mwili wa marehemu na kumwingiza kwenye tumbo la marehemu huyo kuku,kisha wakaaanza kuzika upya", shuhuda aitwaye Sijali Jumanne alisema.

"Kitendo cha ndugu kung'ang'ania kufanya mambo yao,kiliwakera wananchi wakaamua kutoka makaburini,na jeshi la polisi limefika eneo la tukio na kuwakamata ndugu wote wa marehemu",aliongeza shuhuda huyo.

0 comments: