WANNE WAFA AJALINI IRINGA SOMA HAPA KWA HABARI KAMILI

Muonekano wa lori lenye namba za usajili T122 ALW baada ya kugongana na basi la Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD katika Kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo, wilayani Mufindi mkoani Iringa.
 
Basi la Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD baada ya ajali hiyo.
ZAIDI ya watu 4 wamefariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya basi la abiria kutoka Mbeya kwenda Dodoma kugongana na lori katika Kijiji cha Ibetelo eneo la Nyororo wilayani Mufindi mkoani Iringa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Iringa, Ramadhani Mungi amesema kuwa ajali hiyo imetokea saa 4.45 asubuhi na kuhusisha basi mali ya Kampuni ya Fanuel Express  yenye namba za usajili T919 DCD kugongana uso kwa uso na lori lenye namba za usajili T122 ALW mali ya Kampuni ya Transisco lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda nchi jirani.
Amesema watu wawili waliokuwa ndani ya basi wamefariki papo hapo na wote waliokuwa ndani ya lori wanahofiwa kufa, ambapo hadi kufikia  saa 7 mchana, watu wawili ndani ya lori walikuwa wamethibitika kufariki dunia na kufanya waliokufa kuwa wanne.

Zoezi la kuondoa miili iliyokuwa ndani ya lori linaendelea ambapo amesema kuwa huenda idadi hiyo ya waliokufa ikaongezeka.
Akielezea mazingira ya ajali hiyo, Kamanda Mungi amesema kuwa basi hilo lilikuwa likijaribu kulipita basi lililokuwa mbele yake katika eneo ambapo palikuwa na lori lingine lililoharibika, wakati huo huo lori lililohusika katika ajali hiyo lilikuwa likikwepa lori lililoharibika pamoja na basi hilo, ndipo magari hayo yalipogongana uso kwa uso katika jitihada za kukwepana.

Majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa katika Hospitali ya Mafinga, Iringa.

0 comments: