MAMA KANUMBA AGEUKA MBOGO..NI BAADA YA KUULIZWA HATMA YA KAMPUNI YA Kanumba The Great KUFUNGWA
Mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, 'Kanumba The Great', Flora Mtegoa.
KUFUATIA kufungwa
kwa ofisi ya aliyekuwa msanii nyota wa filamu marehemu Steven Kanumba
ya Kanumba The Great, mama mzazi Flora Mtegoa amegeuka mbogo baada ya
kuulizwa kuhusu hatima ya kikazi ya taasisi hiyo.
“Muonekana wa Ofisi ya Kanumba The Great wakati ikiwa inafanya kazi.
Watu
wamezidi kunifuatilia mambo yangu, sitaki kabisa nimechoka, hii kampuni
haimhusu mtu yeyote, hili ni jambo langu siyo lazima niliweke wazi,
kama kampuni imekufa au itaendelea haiwahusu, wanaoamini imekufa waamini
hivyo, maana hata Yesu walisema atarudi hadi leo mbona hajarudi?”
aliuliza kwa hasira mama huyo.
Ofisi
ya mkali huyo wa filamu za Kibongo, aliyefariki ghafla miaka mitatu
iliyopita, ilikuwa eneo la Sinza Mori na ilifungwa wiki mbili
zilizopita, baada ya mama huyo kudaiwa kushindwa kumudu kodi mpya ya
pango ambayo ilipandishwa.
0 comments: