MTOTO WA FLORA SASA JIPU LAPASUKA PWAA!...KILA KITU HADHARANI
Flora Mbasha wakati wa kujifungua.
BAADA
ya utata wa uhalali wa baba wa mtoto wa Mwimba Injili maarufu Bongo,
Flora Mbasha kutawala kwenye magazeti mbalimbali na mitandao ya kijamii,
hatimaye jipu limepasuka baada ya baba mdogo wa Flora,
aliyejitambulisha kwa jina moja la Kisekwa kufunguka kwamba mtoto huyo
ni damu halali ya Mbasha. Kisekwa alifunguka hayo juzikati katika
Mahakama ya Ilala jijini Dar alipokuwa amekwenda kusikiliza kesi ya
aliyekuwa mume wa Flora, Emmanuel Mbasha kudaiwa kumbaka shemeji yake
ambapo alisema anamshangaa Mbasha kushindwa kukiri ukweli ulio wazi
kwamba mtoto ni damu yake wakati moyoni anautambua.
TUJIUNGE NA KISEKWA
“Inakuwaje
Mbasha anashindwa kukubali ukweli kwamba mtoto ni wake wakati anatambua
fika kwamba ujauzito ni mali yake kabla hata ya mgogoro wao? Ndugu wote
tulikuwa tunajua hilo, upande wetu na hata kwao. Mbona hakuikataa tangu
kipindi hicho?
Mgogoro
wao ulikuwa wa mambo ya kawaida ya kifamilia, haukuhusiana hata kidogo
na Flora kuchepuka wala nini, tangu mwanzoni mwa mgogoro wao wakiwa
wanaishi pamoja wameshaitwa mara tatu katika ofisi za Ustawi wa Jamii na
alielezwa kuwa mkewe ni mjamzito, akifahamu ni mali yake na akaonywa
kuwa kitendo cha kuendekeza migogoro ya mara kwa mara kinaweza kumletea
matatizo mkewe na kichanga kilichokuwa tumboni, mbona hakubisha?
Tulikuwa tukijadili matatizo yao na kila mmoja kuweka hoja zake mezani,
hakuna kati yao aliyehusisha mgogoro huo na suala la kuchepuka,” alisema
Kisekwa.
KIAPO CHATAJWA
Kama
hiyo haitoshi, kuonesha ana uhakika na anachokizungumza, Kisekwa
alimtaka Mbasha ajiapize kwa kushika kitabu kitakatifu cha Biblia kama
ana mashaka na ukweli aliouzungumza.
AKERWA NA MADAI YA GWAJIMA
Mzazi
huyo alisema anakerwa zaidi jinsi ambavyo Mbasha amewahi kukaririwa
akimhusisha mkewe kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Mchungaji wa Kanisa
la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kwamba ni baba wa mtoto huyo.
“Anamsingizia
tu baba wa watu (Gwajima) maskini ya Mungu kwa vile hapendi kuona
anavyomsaidia Flora, lakini ukweli Gwajima sisi ni ndugu yetu, mimi G
ananiita baba mdogo kama anavyooniita Flora,” alisema Kisekwa.
Mchungaji Gwajima.
MBASHA ANASEMAJE?
Wanahabari
wetu walipomtafuta Mbasha kuhusiana na ukweli kwamba kichanga ni mali
yake, hakutaka kukubali wala kukataa zaidi ya kupinga suala la ujomba wa
Flora na Gwajima.
“Flora
aseme ukweli, ujomba wa yeye na Gwajima umetoka wapi? Hilo tu ndiyo
nataka alifafanue kwa undani maana wajomba zake wote mimi
nilitambulishwa wakati ninamuoa,” alisema Mbasha.
Mwandishi: Kuhusu ukweli kwamba mtoto ni wako unazungumziaje?
Mbasha: Hilo litajulikana tu lakini mimi nataka kujua ujomba wake na Gwajima umetoka wapi? Hapo tu.
TUJIKUMBUSHE
Mbasha
na Flora ambao waliishi kwenye ndoa na kufanikiwa kupata mtoto mmoja,
mwaka jana walifikia hatua ya kutengana na kila mmoja kuishi kivyake
baada ya kushindwa kutatua mgogoro wao wa muda mrefu wa kifamilia.
0 comments: