Mahakama yatoa siku saba hati ya Halima Mdee kurekebishwa


MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imetoa siku saba kwa upande wa Jamhuri kufanya marekebisho ya hati ya mashitaka katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema (Bawacha), Halima Mdee (35) na wenzake wanane.
 
Hakimu Mkazi Janeth Kaluyenda alitoa amri hiyo jana wakati akitoa uamuzi wa ombi la washitakiwa hao kufutiwa mashitaka. Akitoa uamuzi huo, Hakimu Kaluyenda alisema amesikiliza hoja za pande zote mbili na kupitia kesi mbalimbali hivyo aliamuru hati ya mashitaka ifanyiwe marekebisho ndani ya siku saba.
 
Katika ombi lao washitakiwa kupitia kwa Wakili wao Peter Kibatala waliiomba Mahakama iwafutie mashitaka ya kufanya mkusanyiko usio halali kwa lengo la kutembea kwenda kwenye Ofisi ya Rais kwa kuwa lina mapungufu kisheria.
 
Washitakiwa hao wanakabiliwa na mashitaka, wakidaiwa Oktoba 4, 2014 katika Mtaa wa Ufipa, bila kuwa na uhalali walikiuka amri halali ya kutawanyika iliyotolewa na Mrakibu wa Polisi (SP), Emmanuel Tillf kwa niaba ya Jeshi la Polisi

0 comments: