OHOO! MTUMISHI WA MUNGU ANASWA NA MKE WA MTU INGIA HAPA KWA PICHA NA HABARI KAMILI


Mtumishi Fredrick Kishindo ‘Badoo’ akijistili kwa kanga baada ya fumanizi hilo.

Ohoo, ama kweli dunia imekwisha! Mtumishi wa Mungu (Muinjilisti) ambaye kipindi chake cha dini kinarushwa katika kituo kimoja maarufu cha televisheni Bongo (Jina tunalihifadhi) aliyefahamika kwa jina la Fredrick Kishindo ‘Badoo’ hivi karibuni alipata aibu ya kufungulia mwaka 2015 baada ya kunaswa na mke wa mtu chumbani.
Ilikuwaje?
Awali chanzo cha habari kilichoomba hifadhi ya jina lake kilieleza kuwa, Januari 11, mwaka huu Muinjilisti huyo anayesifika kwa kuhubiri watu waache dhambi alionekana akinyata kuingia kwenye nyumba ya mke wa mtu huyo iliyopo Sinza jijini Dar huku kukiwa na taarifa kuwa, mume wa mwanamke huyo alikuwa safarini.
Wifi mtu atonywa
Ikaelezwa kuwa, kufuatia mazingira hayo wifi wa mwanamke huyo alitonywa juu ya taarifa za Badoo kuingia kwenye nyumba ya kaka yake, maelezo yaliyomshitua hivyo kulazimika kuelekea eneo la tukio.
Baada ya wifi mtu huyo kufika nyumbani kwa kaka yake na kuhakikishiwa kuwa Badoo yuko ndani, aliuliza namna ya kuwapata mapaparazi ambapo mmoja wa majirani alimpatia namba ya simu, akawapigia.
...Akivaa shati huku kitendea kazi chake(Biblia) kikiwa nyuma yake.
Polisi washirikishwa
Katika kuhakikisha usalama katika eneo hilo, wifi huyo pia aliwasimamisha polisi waliokuwa doria na kuwatonya juu ya uzinzi unaofanyika nyumbani kwa kaka yake na kwa kuwa kazi ya askari ni kulinda raia na mali zao, walitoa ushirikiano.
Muinjilisti, mke wa mtu live
Polisi waliongozwa na wifi mtu huyo hadi kwenye chumba ambacho madhambi yalikuwa yakitendeka, walipoingia walikuta mke wa mtu na mtumishi huyo wa Mungu wakiwa kama walivyozaliwa.
Aibu iliyoje!
Baada ya kuona ‘picha imeungua’, mtumishi huyo alisikika akisema kuwa amepata aibu ambayo hakuitarajia huku akiomba asipigwe picha wala kufanyiwa kitendo kibaya bali apewe nafasi ya kujitetea.
Aidha mke wa mtu aliyenaswa akimsaliti mumewe alionekana kutahayari na aliishiwa nguvu zaidi alipomuona wifi yake aliyekuwa amefura ile mbaya.
Mchungaji huyo akijitetea baada ya fumanizi hilo.
Utetezi wa mtumishi wa Mungu
Kufuatia kunaswa huko, Badoo alijitetea kwa kujichanganya, awali alisema aliitwa na mwanamke huyo kwa ajili ya kuongea mambo ya biashara na kwamba eti walivua nguo kutokana na hali ya joto iliyokwemo chumbani humo.
Kana kwamba alihisi kajichanganya, Muinjilisti huyo aligeuza utetezi na kusema aliingia majaribuni baada ya kushawishiwa na ibilisi kisha mwanamke huyo hakumwambia kuwa ana mume.
sikie utetezi wake
“Jamani naomba mnisamehe, si kosa langu bali ibilisi ndiye aliyenishawishi na huyu mwanamke hakuniambia kama ana mume. Hapa aliniita kwa ajili ya biashara flani.
“paparazi nawajueni lakini niko chini ya miguu yenu, naomba msiitoe habari hii mtandaoni ntawapa chochote.
Mke wa mtu akijifunika kwa aibu.

Licha ya utetezi wake huo, mapaparazi walisimamia weledi wa kazi yao na kumweleza kuwa, rushwa kwao ni mwiko, mpaka
 wanaondoka eneo la tukio, mke wa mtu huyo alikuwa akiendelea kumuomba msamaha wifi yake huku Muinjilisti naye akijaribu kutuliza mambo yasifike mbali akidai kuwa, mke wake, ndugu na marafiki wakijua ataaibika.
Ni fundisho
Paparazi limefikia hatua ya kuiandika habari hii ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wamekuwa na tabia ya kuvuruga ndoa za watu ikiwa ni pamoja na kufanya mambo mengine ambayo ni kinyume na maadili. 

0 comments: