Mlinzi kutoka jeshi la Uganda
Hawa askari tuliwaona wakati Diamond Platnumz amewasili Uganda na kupokelewa Airport kwa mbwembwe sana.
Kumbe ulinzi wao uliendelea mpaka siku ya sho ambapo mmoja wao aliwekwa Nje ya chumba cha Diamond na Zari. Ni Mlinzi kutoka jeshi la Uganda akilinda usalama Wa@diamondplatnumz na @zarithebosslady Hii picha akiwa nje ya chumba akiwasubiri wakati wakijiandaa.
Read More »
Aya Sasa Siku Ishafika December 19, ile ahadi ya Ali Kiba imetimia. Video ya “Mwana” iko hapa tayari INGIA HAPA KUICHECK HII SIO YA KUKOSA KUANGALIA
13:26 0 comments
maujanjayamjini.blogspot.com ilikupa kipisi cha video ya ‘Mwana’ ya msanii Ali Kiba, leo iko hapa tayari.
Kazi imefanywa na Godfather wa Afrika Kusini, karibu uinjeoy video hiyo hapa nitafurahi ukiniandikia comment yako.
CLICK HAPO CHINI KUICHECK VIDEO
Read More »
Unaifahamu timu yenye wachezaji wazee kuliko zote England? INGIA HAPA KWA HABARI KAMILI
23:30 0 comments
Barani ulaya kila kitu hutawaliwa na tarakimu ambazo huwakilisha takwimu ambazo huhifadhiwa ili kuweka kumbukumbu ya jinsi ya kuendesha masuala mbalimbali kuanzia siasa , uchumi , biashara binafsi za watu na hata kwenye ulimwengu wa michezo .
Kwenye michezo takwimu ambazo zimezoeleka ni zile za kuonyesha jinsi wachezaji wanavyofanya kazi uwanja kwa maana ya asilia ya juhudi na mahali ambako kocha na wasaidizi wake wa masuala ya ufundi wanaweza kutambua ubora na udhaifu .
Hivi karibui takwimu zimeitaja klabu ya Manchester City kuwa timu ambayo ina wastani wa umri mkubwa kuliko klabu zote zinazoshiriki ligi za soka nchini England .
Takwimu hizi zimeonyesha kuwa Manchester City ina wastani wa umri wa miaka 28.8 kwa wachezaji wake umri ambao ni mkubwa kuliko klabu zote kubwa za ligi tano bora barani ulaya kwa maana ya Epl , Primera Liga , Serie A , Bundesliga na Ligue 1.
Kwa jumla Man City imeshika nafasi ya 7 katika utafiti uliofanyw akwa kutazama wastani wa umri wa wachezaji wa klabu zipatazo 500 barani ulaya kuanzia ligi kuu mpaka madaraja ya chini.
Manchester City ina wachezaji 12 ambao wana umri kuanzia miaka 29 kwenda mbele wakiwemo Kina Martin Demichelis , Frank Lampard ,Bacary Sagna , Yaya Toure , Gael Clichy , Jesus Navas na wengine .

Wachezaji kama Nemanja Vidic wanaifanya Ligi ya Serie A iwe ligi inayoongoza kwa kuwa na wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji.
Kwa upande wa timu ambazo zina wastani wa umri mdogo ni Newcastle United , Manchester United , Southampton , Arsenal na Liverpool .
Ligi ya Italia Serie A inaonyesha kuwa ndio ligi yenye wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji wake huku ligi ya Uholanzi ikionekana kuwa ligi yenye wastani wa umri mdogo kwa wachezaji wa timu zake .
Read More »

Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania bila ubishi wowote ndio klabu bora kwa sasa ulimwenguni kote , hii ni kutokana na aina ya matokeo ambayo wanayapata kwneye mashindano mbalimbali ambayo wanashiriki kuanzia ligi ya Hispania , Kombe la Mfalme , Ligi ya mabingwa barani ulaya na michuano ya kombe la dunia inayoendelea huko nchini Morocco ambako mabingwa hao wa Ulaya wameingia hatua ya Fainali .
Jumla yote Madrid imeshinda michezo 21 katika mashindano yote rekodi ambayo wanazidi kuivunja huku kukiwa hakuna dalili zozote za timu hii kupata matokeo tofauti na ushindi huku wakiwa wamevunja rekodi ya kushinda mechi 18 mfululizo iliyowahi kuwekwa na Barcelona iliyokuwa chini ya Mholanzi Frank Rijkaard katika msimu wa mwaka 2005/06.
Kwa kasi hii rekodi pekee ya kushinda mechi mfululizo iliyobaki kuvunjwa itakuwa ile iliyowahi kuwekwa na Ajax Amsterdam kwenye msimu wa mwaka 1971/72 ambapo timu hiyo ilishinda michezo 26 .
Ubora huu unaonekana kwenye matokeo unatokana na aina ya wachezaji ambao Real Madrid inao wakiongozwa na mchezaji bora kwa sasa Cristiano Ronaldo .
Takwimu kadhaa zinaonyesha kuwa Real Madrid wamekuwa bora kwenye kila idara na ni vigumu sana kuwazuia .
Katika michezo 21 ambayo timu hii imecheza hadi kufikia sasa , imefanikiwa kufunga jumla ya mabao 79 , ikiwa imeruhusu kufungwa mabao 10 pekee .
Katika mabao hayo 79 ambayo Madrid imefunga jumla ya mabao 19 yamefungwa kwa kutumia mguu wa kushoto , mabao mengine 42 yakiwa yamefungwa kwa kutumia miguu ya kulia na mengine 15 yakiwa yamefungwa kwa kicha .
Zaidi ya hapo , mabao 9 yamefungwa nje ya eneo la hatari au kisanduku cha penalty (penalty box) na mabao 70 yakiwa yamefungwa ndani ya eneo hilo na mabao 8 yamefungwa kwa njia ya adhabu ya mkwaju wa penati .
Katika kipindi hiki chote wachezaji kadhaa wamechangia katika mafanikio ambayo Real imeyapata kwenye michezo yake 21 ambayo imeshinda mfululizo kuanzia kwa Cristiano Ronaldo , Gareth Bale , Karim Benzema , James Rodriguez , Toni Kroos, Isco ,Sergio Ramos , Pepe ,na kipa Iker Cassillas ambaye hatimaye amerudisha hadhi yake iliyowahi kutishia kupotea chini ya kocha Jose Mourinho .
Nyuma ya mafanikio yote haya ni kocha Mtaliano Carlo Ancelotti ambaye amefanikiwa kuwafanya wachezaji wote wa Real Madrid kuwa kitu kimoja na kupambana mwanzo mpaka mwisho kuhakikisha wanatimiza lengo ambalo ni kujaribu kuibuka na ushindi kwenye kila dakika 90 wanazokuwa uwanjani dhidi ya wapinzani wa aina tofauti .

Kocha Mtaliano Carlo Ancelotti amefanya kazi kubwa ya kuifanya Real Madrid kuwa timu bora barani Ulaya .
Tarehe | Mpinzani(timu) | Mashindano | Magoli(real) | Magoli(wapinzani) | Umiliki Mpira | Ufasaha wa pasi | Pasi | Mashuti |
---|---|---|---|---|---|---|---|---|
16/09/14 | Basle | Champions League | 5 | 1 | 54.35 | 90.36 | 560 | 17 |
20/09/14 | Deportivo la Coruna | La Liga | 8 | 2 | 59.83 | 91.75 | 679 | 15 |
23/09/14 | Elche | La Liga | 5 | 1 | 64.74 | 90.91 | 660 | 20 |
27/09/14 | Villarreal | La Liga | 2 | 0 | 49.72 | 85.66 | 502 | 7 |
01/10/14 | Ludogorets | Champions League | 2 | 1 | 60.93 | 87.77 | 548 | 15 |
05/10/14 | Athletic Bilbao | La Liga | 5 | 0 | 60.12 | 86.76 | 589 | 19 |
18/10/14 | Levante | La Liga | 5 | 0 | 61.3 | 90.72 | 636 | 17 |
22/10/14 | Liverpool | Champions League | 3 | 0 | 54.17 | 88.38 | 680 | 12 |
25/10/14 | Barcelona | La Liga | 3 | 1 | 42.19 | 85.38 | 431 | 11 |
29/10/14 | Cornella | Copa Del Rey | 4 | 1 | 73.22 | 89.58 | 758 | 11 |
01/11/14 | Granada | La Liga | 4 | 0 | 66.77 | 88.06 | 628 | 15 |
04/11/14 | Liverpool | Champions League | 1 | 0 | 60.13 | 90.99 | 710 | 15 |
08/11/14 | Rayo Vallecano | La Liga | 5 | 1 | 43.83 | 81.38 | 435 | 15 |
22/11/14 | Eibar | La Liga | 4 | 0 | 62.3 | 85.51 | 559 | 17 |
26/11/14 | Basle | Champions League | 1 | 0 | 53.32 | 84.35 | 543 | 6 |
29/11/14 | Malaga | La Liga | 2 | 1 | 57.86 | 88.4 | 474 | 18 |
02/12/14 | Cornella | Copa Del Rey | 5 | 0 | 63.08 | 89.71 | 680 | 10 |
06/12/14 | Celta Vigo | La Liga | 3 | 0 | 48.78 | 81.75 | 389 | 17 |
09/12/14 | Ludogorets | Champions League | 4 | 0 | 61.77 | 91 | 600 | 19 |
12/12/14 | Almeria | La Liga | 4 | 1 | 60.5 | 79.91 | 458 | 12 |
16/12/14 | Cruz Azul | FIFA Club World Cup | 4 | 0 | 58.28 | 89.16 | 609 |
Read More »
HII WATOTO AWARUHUSIWI KUINGIA HAPA CHECK PICHA ZA LAANA ZA UYU MDADA DAH NI HATARI AISEE........!!!!!!!
16:37 0 comments
Utaelewa tu tupo karne ipi na kizazi cha Jina gani.
Je unadhani hizi picha zilikusudiwa au zilipigwa bahati mbaya.

Read More »

Rais Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri Mizengo Pinda amekatiza kwa muda, ziara yake katika Falme za
Kiarabu kwa maelezo kwamba ameitwa nyumbani na Rais Jakaya Kikwete kwa
shughuli maalumu.Waziri Mkuu ambaye yuko katika ziara ya kutembelea nchi za Falme za Kiarabu, ikiwa ni sehemu ya kudumisha ushirikiano na kutafuta wawekezaji, amekatisha ziara hiyo siku mbili baada ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema kujiuzulu kutokana na kashfa ya Escrow.

Waziri mkuu Mizengo Pinda.
Werema alijiuzulu juzi na Rais Kikwete akaridhia hatua hiyo, huku
umma ukisubiri hatua zaidi dhidi ya mawaziri na watendaji wa Serikali
waliotajwa katika sakata hilo.Katika barua yake ya kujiuzulu, Jaji
Werema alisema ushauri wake wa kisheria kuhusu Akaunti ya Tegeta Escrow
haukueleweka na hivyo kuchafua hali ya hewa.Kwa mujibu wa ratiba ya ziara hiyo, leo Waziri Mkuu alitarajiwa kufanya mazungumzo na washiriki wa maonyesho ya B2B pamoja na kutembelea maeneo mengine lakini ziara hiyo imefutwa na badala yake anaondoka asubuhi kurudi nyumbani.Baadaye leo Pinda alitakiwa kwenda Doha, Qatar kwa ziara kama hiyo hadi Desemba 23.
Baada ya kukamilisha jukumu aliloitiwa, Waziri Mkuu anatarajiwa kurejea Falme za Kiarabu Jumamosi kuendelea na ziara yake.
(Chanzo: BBC)
Read More »
breaking news ESCROW: PROF. TIBAIJUKA AKATAA KUJIUZULU..ASEMA KAMA KUJIUZURU NI FASHENI BASI YEYE HAYUKO KIFASHENI
15:40 0 comments
Aongeza kuwa watu wanaona suala la kujiuzulu kama fasheni ila yeye hayupo katika fasheni hiyo.
Read More »
Flora Mbasha, akimbilia mahakama ya kisutu, akiomba kuvunja ndoa kati yake na mumewe Story Kamili Ipo Hapa
15:39 0 comments
Mwimbaji maarufu wa nyimbo za Inili, Flora Mbasha,
amekimbilia mahakama ya hakimu mkazi kisutu, akiomba
kuvunja ndoa kati yake na mumewe, Emmanuel Mbasha.
Flora anadai sababu za kuomba kuvunja ndoa hiyo apewe
talaka ni kutokana na tabia ya mumewe kumpiga,
kumnyanyasa na kushindwa kumpatia matibabu.
Una lipi la kuwaambia wanandoa hawa?
Read More »
CHADEMA YATOA TAMKO: Yaitaka Serikali kuwachukulia hatua waliohusika na wizi wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
10:33 0 comments
Chama
cha demokrasia na maendeleo-Chadema- kimeitaka serikali kuwachukulia
hatua ikiwemo kuwafikisha mahakamani viongozi waliohusika katika wizi wa
fedha katika akaunti ya Tegeta -Escrow- licha ya wengine kuandika barua
kujiuzulu wadhifa zao.
Akizungumza
na waandishi wa habari, naibu katibu mkuu wa Chadema, Mhe.John Mnyika
amemtaka rais Jakaya Kikwete kuyafanyia kazi maadhimio ya bunge ya
kuwaondoa na kuwafikisha katika vyombo vya sheria viongozi hao, hata
kama watajiuzulu nyazifa zao.
Akielezea
uchaguzi wa serikali za mitaa, naibu katibu mkuu wa chama hicho
Zanzibar Bwana Salum Mwalimu amemtaka waziri wa tamisemi Mhe. Hawa
Ghasia kutangaza matokea chaguzi za serikali za mitaa kwa nchi nzima
badala ya kuwahachia viongozi wa vyama vya siasa kuendelea kuwadanganya
wananchi kuwa vyama vyao vimepata ushindi wa kishindo.
Kwa
upande wake baadhi ya wananchi wameitaka serikali kufuatilia ajira za
wageni katika baadhi ya benki nchni kutokana na ongezeko la wizi ambao
yanaambatana na baadhi ya watendaji kujiuzulu nyadhifa zao baada ya
muda.
Read More »
Rais wa Serikali ya wanafunzi UDOM amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wanaojihusisha na ukahaba
10:31 0 comments
Rais wa Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha UDOM Masatu
Kyabwene amekiri kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi wa
vyuo vya elimu ya juu Dodoma kujihusisha na biashara ya
ukahaba kutokana na kukosa mikopo. Akizungumza na paparazi
alisema
“Kuna baadhi ya wanafunzi chuoni kwangu wana maisha magumu
sana kutokana na kukosa mkopo,wakati mwingine wananifuata
mimi na kunielezea shida zao ili niwasaidie,wengine ni yatima
hawana baba wala mama wa kuwalipia ada,siyo siri maisha ya
wanafunzi hawa ni magumu sana”
Tatizo la kucheleweshwa kwa mikopo limekuwa sugu sana katika
vyuo vikuu hapa tanzania ikiwemo chuo cha mzumbe morogoro
ambapo wanafunzi wa mwaka wa pili hawajui hatma yao ya
kupata mkopo tangu wapate matokeo yao ya mitihani.
Read More »
Picha,Mapokezi Ya Diamond Platnumz Uganda , Zari Alimpokea Airport Kwa Njia Hii Ingia Hapa Kuona Kila Kitu....!!
03:01 0 comments
Msanii Diamond Platnumz ameondoka Tanzania leo mchana na kuelekea
Uganda kwaajili ya Party yab Zari The Boss Lady. #ZariAllWhiteCirocParty
inayofanyika Kampala. Hizi ni picha za Diamond alivyowasili kwenye
uwanja wa ndege na kupokelewa na Zari.
Read More »
Read More »
Ingia hapa kuna PICHA jinsi Zari ampokea Diamond Kampala............ jionee hapa!!!
02:55 0 comments
Zari baada ya kumpokea Diamond
Diamond Platnumz ametua Kampala jijini Uganda tayari kwaajili ya kutumbuiza Alhamis hii kwenye show ya Zari All White Ciroc Party jijini humo. Diamond alipokelewa kwenye uwanja wa ndege na mpenzi wake Zari Ttale aka The Bosslady.

Wawili hao wamekutana kwa mara nyingine baada ya hivi karibuni kuwa pamoja kwenye tuzo za Channel O.
Read More »
Ile issue ya Escrow, hii ni taarifa ya Kiongozi mmoja kujiuzulu leo December 16 Soma Hapa Kwa Habari Kamili
21:02 0 comments
Wiki
chache zilizopita wakati Kikao cha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania kikiendelea, macho ya watu wengi na masikio yalikuwa na hamu ya
kutaka kuujua mwisho wa sakata la Escrow.
Wakati watu wengi wakisubiri maamuzi
yatakayotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya
Kikwete kuhusiana na Ripoti juu ya issue ya ubadhilifu wa fedha kwenye
akaunti ya Escrow, leo December 16 kuna taarifa iliyotufikia muda mfupi
iliopita kuhusu kiongozi mmoja wa Serikali kujiuzulu.
Taarifa iliyoripotiwa na kituo cha ITV inasema
aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema
amejiuzulu siku ya leo na barua yake tayari imefika Ikulu ambapo Rais
Kikwete ameridhia maamuzi hayo na kumshukuru kwa uamuzi huo kwa kuwa
ushauri wake kuhusiana na suala la Tegeta Escrow haukueleweka.
Read More »
Sasa ametangaza rasmi kustaafu soka… Na huku ndiko anakoelekea kwa sasa… Ingia Hapa Kwa Habari Kamili
19:29 0 comments
Kwa wale wapenzi wa soka Thierry Henry
sio jina geni kwao, amekuwa nyota ambaye ameng’aa kwenye mchezo huo kwa
muda mrefu sana akichezea vilabu mbalimbali ikiwemo Arsenal na
Barcelona.

Jamaa ametangaza rasmi kustaafu soka
dakika chache zilizopita na kusema kuwa kuanzia mwakani ataanza
kujishughulisha kama Balozi wa Sky Sports huku akisema kuwa anajisikia
furaha kuchezea vilabu vikubwa na pia anaamini anajiunga na kituo
kikubwa cha Television na mattarajio yake ni kuwa mchambuzi bora wa
michezo kwenye kituo hicho.
.@ThierryHenry has retired from football and joins Sky Sports from the start of 2015. #WelcomeThierry https://t.co/KpevkqCMmk
— Sky Sports (@SkySports) December 16, 2014
Read More »
Ni kama vile klabu ya Simba ina mapenzi na taifa la Uganda baada ya klabu hiyo kukamilisha jumla ya wachezaji watano raia wa kigeni ambao wanatoka kwenye taifa hilo la Afrika Mashariki .
Simba imetangaza na kuthibitisha kuwa wachezaji wake watano wa kigeni kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi, Daniel Serunkumma, Simon Serunkumma, Joseph Owino na Juko Mursheed.
Emmanuel Okwi na Joseph Owino ni wawili kati ya wachezaji watano raia wa Uganda walioko Simba.
Wachezaji wawili kati ya hao (Okwi na Owino ) na watatu wengine (Serunkumma Simon, Dany na Juko) wamesajiliwa katika kipindi hiki ambapo dirisha dogo la usajili liko wazi.
Nafasi za wachezaji watatu hao raia wa Uganda zimekuja kujaza nafasi za wachezaji wawili toka Burundi ambao ni Amisi Tambwe na Pierre Kwizera pamoja na Mkenya Paul Mungai Kiongera .
Danny Sserunkumma ni raia mwingine wa Uganda aliyeko Simba.
Kiongera bado ataendelea kuwa mchezaji wa Simba hadi atakapopona jeraha lake la goti ambapo amekwenda kufanyiwa upasuaji nchini India huku Tambwe na Kwizera wakiwa wameachwa moja kwa moja .
Mrundi Perre Kwizera ameachwa baada uongozi wa Simba kutoridhishwa na kiwango chake.
Mkenya Paul Kiongera ameachwa japo Simba itamtumia msimu ujao.
Mrundi mwingine aliyeachwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita Amisi Tambwe.
Simba imetangaza na kuthibitisha kuwa wachezaji wake watano wa kigeni kwa msimu huu ni Emmanuel Okwi, Daniel Serunkumma, Simon Serunkumma, Joseph Owino na Juko Mursheed.
Emmanuel Okwi na Joseph Owino ni wawili kati ya wachezaji watano raia wa Uganda walioko Simba.
Wachezaji wawili kati ya hao (Okwi na Owino ) na watatu wengine (Serunkumma Simon, Dany na Juko) wamesajiliwa katika kipindi hiki ambapo dirisha dogo la usajili liko wazi.
Nafasi za wachezaji watatu hao raia wa Uganda zimekuja kujaza nafasi za wachezaji wawili toka Burundi ambao ni Amisi Tambwe na Pierre Kwizera pamoja na Mkenya Paul Mungai Kiongera .
Danny Sserunkumma ni raia mwingine wa Uganda aliyeko Simba.
Kiongera bado ataendelea kuwa mchezaji wa Simba hadi atakapopona jeraha lake la goti ambapo amekwenda kufanyiwa upasuaji nchini India huku Tambwe na Kwizera wakiwa wameachwa moja kwa moja .
Mrundi Perre Kwizera ameachwa baada uongozi wa Simba kutoridhishwa na kiwango chake.
Mkenya Paul Kiongera ameachwa japo Simba itamtumia msimu ujao.
Mrundi mwingine aliyeachwa ni mfungaji bora wa msimu uliopita Amisi Tambwe.
Read More »
Katika usiku ambao umekuwa na movement nyingi za wachezaji na makocha , klabu ya Simba imekamilisha usajili wa beki wa pembeni toka timu ya Mtibwa Sugar, Hassan Kessy.
Beki huyo ambaye ametokea kuwa mmoja kati ya wachezaji wa kutumainiwa kwenye klabu hiyo ya wakata miwa wa huko Manungu Turiani mkoani Morogoro, anaungana na wachezaji wapya waliosajiliwa katika kipindi hiki cha dirisha dogo ambao ni Simon Sserunkuma, Danny Sserunkuma, na Juko Murshid wote kutoka Uganda.
Kessy ambaye ametajwa kuwa moja kati ya wachezaji wanaokaribia kuwa mmoja ya wachezaji wa Timu ya Taifa Stars alichezea Mtibwa kwa mara ya mwisho katika mchezo wa kirafiki ambao ilifungwa na Azam Fc 3-1.

Beki huyu anasajiliwa baada ya mazungumzo ya muda mrefu yaliyofanyika chini ya usimamizi wa viongozi wa Simba wakiongozwa na Geoffrey Nyange Kaburu na Kiongozi wa Mtibwa, Jamal Bayser.
Tetesi zaidi zinasema kuwa Simba imemsajili beki huyo kwa thamani ya shilingi milioni 30.
Read More »
Moja ya vichwa vya habari vilivyokuwa vimepambwa na habari kumhusu Emerson.
Taarifa za usajili na kuachwa wachezaji zinazidi kuingia na safari hii inasemekana kuwa kiungo Mbrazil Emerson amekuwa mhanga wa kwanza wa kuondoka kwa kocha Mbrazil Marcio Maximo baada ya mchezaji huyo kuachwa na Yanga.
Mbrazil huyo anaondoka Yanga baada ya kucheza mechi moja pekee dhidi ya Simba ambako Yanga ilifungwa 2-0.
Emerson alishindwa kuwaridhisha mashabiki wa Yanga ambao wengi walionyesha kukerwa na uwezo mdogo wa kiungo huyo katika dakika 45 alizocheza kwenye mechi dhidi ya Simba.
Emerson alikuja nchini siku chache zilizopita ambapo alipaswa kuziba nafasi iliyoachwa wazi na mshambuliaji Genilson Santos Santana Jaja ambaye hakurudi baada ya kuondoka nchini kufuatia kusimama kwa ligi.

Read More »
Subscribe to:
Posts (Atom)