DIAMOND PLATNUMZ ASHIRIKI PROJECT YA EBOLA


Nyota wa muziki Diamond Platnumz ambaye mwishoni mwa wiki ameweza kushinda tuzo tatu huko Afrika Kusini, amekuwa ni moja kati ya wasanii wakubwa Afrika walioshiriki katika project ya pamoja inayokwenda kwa jina We are the World Africa.


Kazi hii kubwa imefanyika huko Afrika Kusini ikiwashirikisha pia mastaa kutoka nchi nyingine za Afrika kama vile Banky W, Mafikizolo, Iyanya, Don jazzy na wengineo wengi.
 
Kabla ya kuondoka Tanzania Diamond aliiambia Mpekuzi juu ya ushiriki wake katika project hiyo kubwa, ikiwa pia na lengo la kuongeza uelewa juu ya Gonjwa la Ebola ambalo limekuwa tishio nchi za Afrika Magharibi na Afrika kwa ujumla.

0 comments: