
Barani ulaya kila kitu hutawaliwa na tarakimu ambazo huwakilisha
takwimu ambazo huhifadhiwa ili kuweka kumbukumbu ya jinsi ya kuendesha
masuala mbalimbali kuanzia siasa , uchumi , biashara binafsi za watu na
hata kwenye ulimwengu wa michezo .
Kwenye michezo takwimu ambazo zimezoeleka ni zile za kuonyesha jinsi
wachezaji wanavyofanya kazi uwanja kwa maana ya asilia ya juhudi na
mahali ambako kocha na wasaidizi wake wa masuala ya ufundi wanaweza
kutambua ubora na udhaifu .
Hivi karibui takwimu zimeitaja klabu ya Manchester City kuwa timu
ambayo ina wastani wa umri mkubwa kuliko klabu zote zinazoshiriki ligi
za soka nchini England .

Manchester City imetajwa kuwa klabu yenye wachezaji wenye umri mkubwa kuliko wote nchini England.
Takwimu hizi zimeonyesha kuwa Manchester City ina wastani wa umri wa
miaka 28.8 kwa wachezaji wake umri ambao ni mkubwa kuliko klabu zote
kubwa za ligi tano bora barani ulaya kwa maana ya Epl , Primera Liga ,
Serie A , Bundesliga na Ligue 1.
Kwa jumla Man City imeshika nafasi ya 7 katika utafiti uliofanyw akwa
kutazama wastani wa umri wa wachezaji wa klabu zipatazo 500 barani
ulaya kuanzia ligi kuu mpaka madaraja ya chini.
Manchester City ina wachezaji 12 ambao wana umri kuanzia miaka 29
kwenda mbele wakiwemo Kina Martin Demichelis , Frank Lampard ,Bacary
Sagna , Yaya Toure , Gael Clichy , Jesus Navas na wengine .

Wachezaji kama Nemanja Vidic wanaifanya Ligi ya Serie A iwe ligi inayoongoza kwa kuwa na wastani wa umri mkubwa kwa wachezaji.
Takwimu hizi zinaonyesha kuwa Manchester City kwa timu za England
ndio timu yenye wachezaji wenye umri mkubwa kuliko zote huku ikifuatiwa
na Cyrstal Palace , Stoke City,West Bromwich Albion na QPR .
Kwa upande wa timu ambazo zina wastani wa umri mdogo ni Newcastle
United , Manchester United , Southampton , Arsenal na Liverpool .

Ligi ya Uholanzi inaongoza kwa kuwa na wachezaji wenye wastani mdogo kwenye umri .
Ligi ya Italia Serie A inaonyesha kuwa ndio ligi yenye wastani wa
umri mkubwa kwa wachezaji wake huku ligi ya Uholanzi ikionekana kuwa
ligi yenye wastani wa umri mdogo kwa wachezaji wa timu zake .