PAC yaibua ufisadi wa bilioni 9/- katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere JNIA
Kamati
ya Kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imeibua ufisadi uliopelekea
upotevu wa zaidi ya Shilingi bilioni tisa katika Uwanja wa Ndege wa
Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), jijini Dar es Salaam.
Akiwasilisha
taarifa ya mwaka ya Kamati hiyo kuhusu hesabu zilizokaguliwa za
Serikali Kuu na Mashirika ya Umma kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30,
2013, Mwenyekiti wa PAC, Zitto Kabwe alisema kuwa ufisadi huo umetokea
kwenye mradi wa ujenzi wa Jengo la watu mashuhuri kwenye uwanja huo.
Zitto
alisema kuwa ukaguzi uliofanyika unadhihirisha kwamba harama halisi za
ujenzi wa jengo la watu mashuhuri kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius
Nyerere zina mkanganyiko.
Alisema
katika ukaguzi ulofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Fedha za
Serikali (CAG), mkaguzi huyo alishindwa upata nyaraka wala vilelezo
vyote vilivyomo kwenye majalada ya ofisi za Mamlaka ya vya Ndege (TAA)
na yale ya kiwanja cha JNIA ikiwemo mkataba kwa ajili ya kuonyesha
gharama halisi za ujenzi huo.
Alisema kuwa kilichopatikana ni ‘offer for Grant for VIP Launge’ yenye thamani ya fedha za kitanzania shilingi bilioni 5.3.
Zitto
alisema kuwa ili thamani ya ujenzi wa jengo hilo, CAG aliagiza Wizara
ya Uchukuzi iwasiliane na mthathimini Mkuu wa Majengo ya Serikali ili
afanye thathmini ya thamani ya jengo hilo.
“Kwa
mujibu wa taarifa ya Mthamini Mkuu wa Majengo ya Serikali hadi kufikia
mwezi Mei, 2014 gharama za ujenzi wa jingo hilo zilikuwa ni Shilingi
bilioni tatu na mchango wa Serikali kwa shughuli zilizohusu ujenzi wa
jengo hilo ulikuwa ni Shilingi milioni 869.4 tu.
Alisema
kuwa hata hivyo katika mikutano mbalimbali ya bunge kati ya mwaka 2011
na 2012, Serikali ilitoa tamko kuwa jengo la watu mashuhuri katika
Uwanja wa Ndege wa Dar es Salaam kuwa ni jumla ya shilingi bilioni 12!
Zitto alisema kuwa tamko hilo la Serikali ni tofauti ya shilingi bilioni
tisa zaidi ya kiwango cha Mthamini Mkuu wa Serikali, hali ambayo
inaonyesha kuna matumizi yasiyo ya kawaida ya fedha hizo.
0 comments: