
DUNIA imekwisha!
Wasichana wawili warembo, Maua Sadick (24), mkazi wa Stakishari, Ukonga
wilayani Ilala na Lucy Fred (23), mkazi wa Karakata jijini Dar es
Salaam, wanashikiliwa katika Kituo cha Polisi Stakishari, Ukonga, Dar
kwa kesi yenye jalada STK/RB/463/2015 wakidaiwa kufanya mapenzi ya
jinsia moja.
Warembo, Maua Sadick (mwenye shati la draft) na Lucy Fred wakipozi kimahaba.
Warembo
hao walikamatwa Januari 12, mwaka huu saa sita mchana, nyumbani kwa
Maua wakidaiwa kufanya ngono kinyume cha sheria ya kujamiiana ambapo
watu wa jinsia moja ni makosa kukutana kimwili.
NDUGU, MAJIRANI WAKERWA
Kwa
mujibu wa habari za kipolisi, kukamatwa kwa Maua kulitokana na taarifa
za baadhi ya ndugu na majirani zilizopelekwa polisi kwamba, wasichana
hao wanapokuwa kwenye tendo la ndoa wamekuwa wakipiga kelele za
udhalilishaji kwa familia zao.
Wasichana hao wakiwa maeneo tofauti.
WALISHAONYWA, HAWAKUSIKIA
Vyanzo
makini kutoka jirani na makazi ya Maua vinadai kuwa, kutokana na hali
hiyo, baadhi ya watu walijitolea kuwaonya wasichana hao kuwa na staha
wawapo kwenye faragha yao lakini pia wao ni wanawake haiwezekani wacheze
mchezo huo wenyewe kwa wenyewe lakini hawakutaka kusikia.
MAJIRANI WAFUNGULIA REDIO SAUTI YA JUU
“Ilifika
mahali wakiingia chumbani kuanza mambo yao sisi majirani tunazidisha
sauti za redio ili watoto wasisikie lakini na wao sauti zao zinakuwa juu
kushinda za redio,” alisema jirani mmoja akiomba jina lake lifichwe ili
kukwepa uhasama.
Alisema
kutokana na hali hiyo waliamua kufikisha habari hizo polisi kwani ni
kinyume cha sheria watu wa jinsia mmoja kukutana kimapenzi.
Mrembo Lucy Fred ambaye ni mpenzi wa Maua Sadick.
HISTORIA YA LUCY
Wakizidi
kuzungumza na paparazi, majirani hao walisema, Lucy ambaye ndiye
anaitwa mke na Maua amekuwa akitoka nyumbani kwa wazazi wake Karakata
kwa lengo la kumfuata Maua.
SIKU YA TUKIO
Ilisemekana
kuwa, siku ya tukio, majirani walipoanza kusikia ‘zile sauti zao’,
waliwapa polisi namba ya simu ya mtu wa jirani na Maua kwa lengo la
kusaidia kufika nyumbani hapo.
“Polisi
walipofika waligonga mlango kwa muda mrefu bila kufunguliwa na kelele
za mahaba zilizidi kusikika. Baadaye, nadhani wakati wanapumzika sasa,
Maua alifungua mlango mkubwa na kukutana na macho ya polisi, wakambana
na kumtaka waende wote alipo Lucy, wakaenda chumbani na kumkuta.
“Pia polisi walikuta kidude ambacho huwashwa kwa betri kilichodaiwa pia hutumika wakati wa tendo,” kilisema chanzo.
Warembo hao kama wanavyoonekana kwenye picha zao za instagram.
HISTORIA YA MAUA
Maua
ni binti ambaye ni yatima, amekuwa akiishi mwenyewe kwenye nyumba hiyo
kubwa ya familia hivyo kumwita Lucy mara kwa mara kwa madai ya kufanya
ufuska huo kwa vile wana uhuru.
Inasemekana kuwa, Maua siku zote amekuwa akivaa mavazi ya kiume licha ya kwamba, ni mwanamke kamili.
POLISI WASHANGAA
Taarifa
kutoka vyanzo vya ndani ya jeshi la polisi zinadai kwamba, hata wakiwa
mahabusu ya kituo hicho, wawili hao wamekuwa wakioneshana mapenzi baina
yao kitendo kilichowashangaza mahabusu wengine na polisi pia.
Paparazi
kama kawaida yake ilifika nyumbani kwa Maua na kukutana na mdogo wake
aitwaye Aziz ambaye alikiri kukamatwa kwa Maua na kwamba tangu akamatwe
hajarudi na wala hajui kinachoendelea huku akisema asingependa
kuzungumzia suala hilo kwa sababu ya kutupiwa lawama na wanandugu kwamba
yeye ndiye aliyepeleka taarifa polisi.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki.
“Mimi
sikai hapa, nimefika hivi karibuni nikitokea mkoani. Ndugu wananituhumu
mimi kuita polisi, sijui mtu aliyewapa askari namba yangu wakanipigia
kama wageni wanaokuja nyumbani, nikawapa ramani na walipofika ndipo
nikagundua ni askari,” alisema Aziz.
Mwenyekiti
wa Serikali ya Mtaa, George Mtambalike alipohojiwa na paparazi ofisini
kwake alithibitisha kukamatwa kwa wasichana hao kwa madai ya kufanya
mapenzi ya jinsia moja na aliwatembelea Kituo cha Polisi cha Stakishari.
Kamanda wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, SACP Mary Nzuki alikiri kukamatwa kwao na akasema uchunguzi unaendelea.